Kwani we ni nani?

Kwani we ni nani?
Wakuniekea masharti,
Wakinishika mashati

Kwani we ni nani?
Wakuniget mtaani,
Wa kuniletea muadhara hadharani!

Kwani we ni nani?
Wa kunisetia keja nareh,
Kunimwagia unga kwako ni hareh!
Hata ka kwetu ni mathare

Kwani we ni nani?
Umenyara brotherngu,
Umekuta sistangu, mathangu,
Kila kitu yangu!

Kwani we ni nani?
Kunitangaza mitaani,
Yaani ka simimi huna vibe?
Kwako mi ni ka nyani nini?
Napoanga mwitu bila amani,
Fanya kile unataka kwani!

Kwani we ni nani?
Huna stori isipokua zangu mtaani?
Na stori zako we fala ni pandisa,
Masengenyo pang’ang’a ndiozako!
Mi nikeroma kwako,
Ukisikia kinenge unanibonga unashiba,
Huchoki na petho zako za peni mbili
Kutafuna usinadi ndio wewe!


Kwani we ni nani?
Kunikalia ka stool,
Ni vile umenona manyama kila kona,
Akili ya wery tama ya fisi,
Na ka si mimi,
Hungekua hapo
Ka simimi,
Kwako kungeburn tenne,
Kwako wangetaki tenne,
Ka simimi
ungekua akitembea ka clutch iko ndani?

Kwani we ni nani?
Ni fight Babylon tena wewe,
Yaani unanikazia maright muadhara,
Kunichomea wire kila time,
Ukiniona unavutia wasinadi wire,
Kerende yangu yote wako mazabe,
Juu yako to,
Hutaki kuona mtu ako mbele,
Kila mtu akitoboa unamwondoa ati ni dingo,
Ati siku hizi ye ni poko na nihassle,
Unaingia kwa bash bila invitation!

Kwani we ni nani?
Na kanimakosa si watu huambiwa?
Ndio tuambiane ezah,
Tuchapiane tuelewane?
Ka ni dhuluma nikome,
Ama nitakuamulia roho juu,
Nikukute huko uliko nikuache umejuta
Juu mi ni ukuta unanikuta unajivunja!

1 comment:

Njoki said...

Na hapa ulikuwa unapigana na nani?