Huyu ni shujaa!

Pole pole akatambaa,
ja mnyoo afanyavyoo
Kunyata akaendelea,
kama mwizi atendavyo,
Katikati ya vichaka…
akapita akitetema

Mgongowe umechoka,
akazidi kuinama
Mchachato mchachato,
mwendowe wa kuvizia.
Akiogopa vimoto,
ambavyo zamgoja

Kakaribia ukutani,
akawa kichungulia
Kuna nini? Kuna nini?
Swali lika mlemea,
Lakini akajikaza,
akijua yu shujaa!

Hakuwacha kupeleleza,
ingawa akihofia
Kabaki kuchungulia,
huku moyowe kimpwita

Rafiki tamgundua?
Aweze kumfuata,
Au taona adui,

wa kumfanya asusa!

No comments: