UNGA

Hii shairi niki-i-tunga,
Kwa  port kuna Meli ya unga!
Imetia nanga,na  imechungwa,
Brathee angalau ka-unga.

Round hii hakuna ku-unga
Juu kwa shelf hakuna unga,
Kejani pia wanadai unga!

Imeshakua kama ile unga-
Ya deal za backdoors na dark alleys,
Wanauza hii unga,
Vako ya el-chapo!

Kuna wasee in dark suits na madigaga,
Wameji-pin na ma Uzi na ma Ceska,
Wako mraa na ma big-fish,
Wakiuzia  raiyaa unga!

Kwa silo hakuna grain,
Cartels zime drain,
Na makata za, hakuna rain!

But iko kwa ma-warehouse na wamefunga,
Juu  ndani kuna unga,
Hadi kinenge sasa inadunga!


So bei  ishakua ingine,
Kuna wale wata-omoka
Na wale wata-toboka!

Ukishiba na sembe,
Wengine wanameza wembe,
Kwa shamba wameficha hadi jembe!

Jaribu kuzusha juu ya hii unga,
Hawa ma-dealer watakufunga,

Juu system- hao ndio wali-tunga.

No comments: